Falsafa ya Udereva wa Kujihami
Falsafa ya Udereva wa Kujihami

Ajali nyingi zinaweza kuzuilika kwa kutumia falsafa ya udereva wa kujihami. Lakini swali ni je, nini maana ya udereva wa kujiahami? Zipi kanuni za udereva wa kujihami na ni kitu gani kinamtambulisha dereva anaetumia falsafa ya udereva wa kujihami? Kwa leo tujifunze kuhusu maana ya udereva wa kujihami na sifa za dereva anaetumia falsafa ya udereva wa kujihami. Katika makala zijazo tutaangalia kanuni za udereva wa kujigami. 


  Maana ya Udereva wa Kujihami 

 Ni udereva wa kuzuia ajali zote zinazozuilika, hata zile ambazo zingetokea kwa makosa ya wengine au hali zisizo kubalika 


  Sifa za Dereva anaetumia Falsafa ya Udereva wa Kujihami

  1. Ni dereva anaejituma kuzielewa na kuziheshimu sheria kanuni na taratibu za usalama barabarani
  2. Ana uwezo wakuendesha magari matatu kwa wakati mmoja awapo barabarani. Yaani gari la mbele yake, lakwake na gari lililopo nyuma yake
  3. Haendeshi chombo cha moto katika hali zinzaoweza kusababisha ajali kwake mwenyewe na watumiaji wengine wa barabara
  4. Hatoi mwanya kwa watumia barabara wengine kuhatarisha maisha yake
  5. Muda wote yupo macho na matendo ya watumia barabara wengine na huchukua hatua zinazo stahili kuzuia ajali isitokee
  6. Muda wote yupo tayari kutoa nafasi kwa watumia barabara wengine na huchukua hatua zinazo stahiki ajali isitokee
  7. Muda wote yupo tayari kutoa nafasi kwa watumiaji wa barabara wengine wasio wajibika barabarani
  8. Yupo tayari kutoa haki yake kwa watumia barabara wengine ili kuzuia ajali isitokee.
  9. Ni mvumilivu wa kero za watumia barabara wengine na huchukulia swala hilo kama sehemu ya kawaida ya udereva, muda wote yupo macho na hali zisizo kubalika.
  10. Ni dereva ambae haruhusu umakini wake kuchukuliwa na vizuizi kama matumizi ya simu wakati wa kuendesha, watoto, kula na matumizi “ya make up”

Shirika La Elimu ya Utekelezaji wa Sheria