PROACTIVE LAW ENFORCEMENT FOR SAFE COMMUNITY Jamilifu
Jamilifu

Uhalifu unatendeka katika jamii na wanajamii. Wahalifu ni sehemu ya watu katika jamii ambao kwa namna moja au nyingine (kwa kujua au kutokujua) wanakiuka taratibu ambazo jamii imejiwekea. Jamii hujiwekea taratibu na miongozo maalumu ili kudhibiti tabia na mienendo ambayo inaweza kupelekea uvunjifu wa amani. Kwakua wahalifu wanatoka katika jamii, ni jukumu la jamii husika kubainisha uhalifu na wahalifu na kuwatolea taarifa kwa vyombo vyenye dhamana kisheria. Kwa minajili hiyo, usalama wa jamii upo mikononi mwa jamii husika. 

 
Katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, inatoa wajibu kwa kila mtanzania, kujilinda na kulinda jamii yake, kulinda mali za umma, mali binafsi, mipaka ya nchi na usalama wa nchi kiujumla (Ibara: 27,28 na 146). Ili kuhakikisha wajibu huu unatekelezeka jamii inahitaji kuuelewa uhalifu na madhara yake pamoja na kuzielewa sheria, kanuni na taratibu kwa lengo la kuchochea uhiari katika utekelezaji wa sheria. 
Katika kutambua umuhimu wa juhudi za pamoja kwenye kutokomeza uhalifu jeshi la polisi linaeleza “Mapambano dhidi ya uhalifu ni jukumu la pamoja kati ya Jeshi la Polisi, raia na wadau wengine ili kuweza kuushinda uhalifu wa aina zote".
Kama asasi ya kiraia, PESACO inaelimisha jamii juu ya uhalifu na athari zake kwakua tunaamini uelewa na ushirikishwaji wa jamii utaongeza ufanisi kwenye kutambua, kuzuia na kusuluhisha matitizo ya uhalifu na hofu ya uhalifu.   

 Njia Tunazozitumia Kutoa Elimu
  1. Kushirikiana na serikali za mitaa na vikundi vya polisi jamii ili kuhakikisha jamii inapata elimu juu ya umuhimu wakujilinda na kubainisha uhalifu na wahalifu katika mitaa yao.
  2. Kushiriki na kuomba nafasi yakutoa elimu kwenye mikutano ya vijiji na mitaa
  3. Kuandaa miradi yakufika kwenye kaya hadi kaya kufikisha elimu stahiki
  4. Kuandaa semina za elimu kwa wananchi na watumishi wa serikali;
  5. Kushirikiana na tasisi binafsi zenye malengo yanayofanana;
  6. Kushirikiana na serikali pamoja na taasisi zake (mf. Polisi)
  7. Kuandaa vitabu, makala na vipeperushi elimishi;
  8. Kutumia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari
  9. Kuchapisha makala elimishi katika tovuti ya PESACO