Usalama barabarani umesimama kwenye nguzo kuu tatu ambazo ni:-
- Ubora na uzima wa barabara (Engenering)
- Usimamizi wa sheria za barabara (Enforcement)
- Elimu ya usalama barabarani (Education)
- Kukuza maarifa na uelewa wa sheria za barararani na mazingira yake
- Kuongeza ujuzi kupitia mafunzo na uzoefu
- Kuimarisha na kusisitiza mitazamo chanya wakati wa kutafsiri mazingira hatarishi barabarani, kujilinda binafsi na kuwalinda watumiaji wengine wa barabara
- Kufika kwenye shule za msingi na sekondari kwa lengo la kuwapa wanafunzi na walimu elimu, ujuzi na maarifa ya usalama barabarani.
- Kufika kwenye vituo vya bodaboda na bajaji na kutoa elimu ya usalama barabarani
- Kufika kwenye vituo vya mabasi na daladala kwa lengo la kutoa elimu kwa abiria pamoja na madereva
- Kufika ofisi za serikari na binafsi kwa lengo la kutoa vitabu, nakala na vipeperushi vya usalama barabarani
- Kuandaa mabonanza ya michezo kwa madereva wa bajaji na bodaboda kwa lengo la kuhimiza ushirikiano na umoja kati yao wenyewe na jamii inayowazunguka hasa kwenye swala la usalama barabarani
- Kuandaa, vitabu, nakala na vipeperushi vya usalama barabarani
- Kutumia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari