Redio na televisheni ni njia mojawapo tunayoitumia PESACO kutoa elimu ya usalama barabarani. Njia hii inasaidia sana kurahisisha shuguli zetu na pia inasaidai kuifikia hadhira kubwa kwa wakati mmoja. Tukumbuke kuwa sheria ya usalam barabarani inatambua makundi sita ya watumia barabara, ambayo ni watembea kwa miguu, madereva, abiria, wapanda baiskeli, wapanda pikipiki na wasukuma mikokoteni. Hivyo kwa kutumia media campaign tunafanikiwa kufikai karibu makundi yote. Mpaka sasa tumefanikiwa kufanya media campaign kwenye vituo mbali mbali vya redia mfano TBC FM, KISS FM, CAPITAL REDIO Na UHURU REDIO. Lakini pia tumefanikiwa kufanya kipindi kwenye televisheni, mfano televishen ya CHANEL 10
Tumefanikiwa kutoa mada mbali mbali katika redia na televisheni, mada zinazolenga kundi moja moja na mada za jumla. Mada tulizofanikiwa kutoa ni kama
- Udereva wa kujihami
- Haki na wajibu wa mwenda kwa miguu
- Haki na wajibu wa dereva.