PROACTIVE LAW ENFORCEMENT FOR SAFE COMMUNITY MKINGE MWANAFUNZI DHIDI YA AJALI BARABARANI
MKINGE MWANAFUNZI DHIDI YA AJALI BARABARANI
kampeni hii inalenga  kuhakikiasha wanafunzi hasa wa shule za msingi na sekondari wanapata elimu stahiki ya usalama barabarani. Malengo hasa ya PESACO kuanzisha kampeni hii ni;
  1. Kuwajengea wanafunzi tabia na desturi za kuzifahamu, kuziishi na kuzitekeleza sheria, taratibu na kanuni za usalama barabarani tangu wakiwa wadogo
  2. Kuzifahamu na kuzitumia ipasavyo alama na michoro ya barabarani
  • Kuimarisha na kusissitiza mitazamo chanya wakati wa kutafsiri mazingira hatarishi barabarani,
  1. Kuwajengea wanafunzi uwezo wa kujilinda binafsi na kuwalinada watumiaji wengine wa barabara pindi wawapo barabarani.
Ili kufanikisha malengo hayo manne ya kampeni hii PESACO inatembelea shule za msingi na za sekondari (kwa sasa za mkoa wa dar es salaam) kwa lengo la kuendeleza na kusisitiza elimu ya usalama bararbarani. PESACO inaamini kwamba watoto na vijana ni viongozi na madereva wa kesho, hivyo ni shabaha sahihi kuwekeza mda na maarifa kwao ili baadae waweze kuwa mabalozi wazuri katika swala la usalam barabarani. Mpaka leo tarehe 1-09-2021 shirika limefanikiwa kutoa elimu na mafunzo kwa wanafunzi wasiopungua elfu tatu na mia moja na hamsini wa shule za msingi (3150). Kampeni hii ni endelevu na ni matamanio ya shirika kufikisha elimu hii kwa wanafunzi wote nchi nzima.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *