ELIMU KWA MADEREVA BODABODA NA BAJAJI
ELIMU KWA MADEREVA BODABODA NA BAJAJI
Waendesha pikipiki za magurudumu mawili al maarufu kama bodaboda na pikipiki za magurudumu matatu al maarufu kama bajaji ni kikundi mojawapo katika makundi ya usalama barabarani. Sisi kama shirika tuna program za kuwatembelea katika vituo vyao na kuwapatia mafunzo na elimu ya uslam baranarani. Kwa mfano tarehe 10-4-2021 timu ya PESACO ilitembelea kikundi cha madereva bodaboda na bajaji kituo cha kimara baruti. Siku hiyo madereva hao walipata elimu juu ya umuhimu wa kuendesha pikipiki ukiwa umevaa kofia ngumu au helment. Lakini pia elimu ya sharia ya usalama bararani ilitolewa kwa kuwaelezea na kuwafafanulia vifungu vya sharia has vile vinavyokataza uendeshaji wa mwendo kasi, kuendesha kwa hatari na uzembe pamoja na vifungu vinavyomtaka dereva bodaboda au bajajai kubebe leseni na nakala ya kadi ya chombo chake.

One thought on “ELIMU KWA MADEREVA BODABODA NA BAJAJI

  1. kwa kweli kwa upande wangu nampongeza sana kamanda Swai kwa kazi kubwa anyaofanya ya kuelimisha hawa ndungu zetu madereva wa bodaboda Ambao kwa kweli imekuwa ni changamoto sana haswa pale wanapokuwa wakaidi wa kutumia Alama za barabarani na kufuata sheria za usalama, mfano kupakia mishikiaki, kutokuvaa kofia ngumu, wakati mwingine hawavai viakisi mwanga, Kwakweli ni changamoto sana. Nikupongeze sana Kamanda swai na timu yako kwa kazi kubwa mnayoifanya.. mungu awabariki nyote

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Shirika La Elimu ya Utekelezaji wa Sheria