Uvaaji wa Mkanda wa Usalama kwa Mama Mjamzito
Uvaaji wa Mkanda wa Usalama kwa Mama Mjamzito
Kumekuwa na mkanganyiko juu ya namna na uvaaji wa mkanda wa usalama kwa wanawake wajawazito. Wengi hudhani si vyema kwa mwanamke mjamzito kuvaa mkanda wa usalama kutokana na hali yake. Lakini sihivyo, ni muhimu sana kwa mwanamke mjamzito kuvaa mkanda wa usalama katika hali ambayo itamuweka salama yeye pamoja na mwanae alie tumboni. Kuvaa mkanda wa usalama kunamsaidia mama na mtoto wake alie tumboni kukwepa au kupunguza  madhara ambayo yanaweza kutokana na ajali. Vaa mkanda wa usalama muda wote ukiwa unaendesha gari na kama umepata ajali hata kama ni ndogo nenda kwa daktari haraka iwezekanavyo na hakikisha kama mtoto wako yupo salama na wewe pia. Namana nzuri na sahihi ya mama mjamzito kuvaa mkanda wa usalama akiwa ndani ya gari
  1. Njia salama ya kuvaa mkanda wa usalama ni kuvaa mkanda wa mapaja na mabega kwa pamaoja na hakikisha inakushika vizuri.
  2. Mkanda wa mapaja utaufunga chini ya tumbo ukipita na kukaa vizuri kwenye nyonga na kugusa mapaja. Usivae mkanda huo juu au kwenye tumbo lako
  • Pitisha mkanda wa mabega katikati ya maziwa kuelekea pembeni mwa tumbo lako na usiweke mkanda wa mabega chini ya mkono na hakikisha mkanda haufikii kwenye shingo
  1. Kama utapwaya na kutoka pahala pake, rekebisha ili ukushike vizuri.
Ziada
  • Jizuie
Jaribu kujizuia kutoendesha gari zaidi ya masaa 5 mpaka 6 kwa siku. Kuendesha gari kunachocha kwa kila mtu, na weka akilini kwamba wewe ni mjamzito.
  • Usizime mifuko ya hewa
Kama gari lako lina mifuko ya hewa usiizime mbadala wake jaribu kusogeza kiti chako kutoka kwenye dashibodi  na sogea nyuma uwezavyo au kifua chako kiwe angalau nchi 10 kutoka kwenye dashibodi au usukani. Ukisha fanya hivyo hakikisha bado unaweza kufikia kichapuzi, breki na clutch vizuri bila shida yoyote, pia  ni vizuri kuangalia vioo kuona kama bado unaona vizuri.
  • Kuwa makini na hali yako (unajihisije)
Kama unahisi umechoka, au hali ya hewa sio nzuri kwako, pumzika na kunywa kinywaji ila sio pombe, usiendeshe gari mpaka pale utakapojisikia vizuri.
  • Kaa kwenye kiti cha abiria
Wakati mimba ikiendelea kukua na tumbo lako linakuwa kubwa jaribu kukwepa kuendesha gari,  ni salama zaidi kukaa kwenye kiti cha abiria, acha mtu mwingine aendeshe gari kwa niaba yako awe ni mmeo, ndugu yako, mwanao mwenye vigezo vya kuendesha gari, rafiki yako au dereva wako.

5 thoughts on “Uvaaji wa Mkanda wa Usalama kwa Mama Mjamzito

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

PESACO TANZANIA