Mpanda Pikipiki
Mpanda Pikipiki

Wapanda baiskeli ni miongoni katika makundi sita ya watumia barabara. Wana haki sawa ya kutumia barabara kama ilivyo kwa watembea kwa miguu, watumia vyombo vya moto na abiria. Pia, wana wajibu wakufuata na kuheshimu sheria, taratibu na kanuni za matumizi salama ya barabara. 

 

Je ni mambo gani mpanda baiskeli anapaswa kuzingatia awapo barabarani?

  • Kabla yakuondoka na kuingia barabarani, hakikisha afya yako ipo imara. Usafiri wa baiskeli unategemea nguvu za mwenseshaji, hivyo afya njema ya mwendeshaji ni muhimu ili kuikamilisha safari pasina madhara.
  • Kagua baiskeli yako vizuri ili kuhakikisha ipo katika hali salama itakayo kamilisha safari yako. Katika ukaguzi hakikisha matairi yana upepo wakutosha, mfumo wa breki unafanya kazi vizuri, kengele pamoja na taa.
  • Vaa kofia ngumu kichwani. Kofia ngumu itakusaidia kupunguza madhara ya ajali hasa maeneo yakichwani endapo ajali itatokea.
  • Zingatia swala la mavazi. Vaa viakisi mwanga mbele na nyuma ili kuongeza uonekanaji wako kwa watumiaji wenginge wa barabara hasa nyakati za usiku.
  • Fuata sheria, taratibu na kanuni za barabarani ili kujilinda na kujikinga na ajali.
  • Jali watumiaji wengine wa barabara, mfano watembea kwa miguu. Kumbuka kwamba wana haki yakutumia barabara kama wewe.
  • Tembea upande wakushoto wa barabara kama ilivyo kwa vombo vya moto. Bana upande wa kushoto zaidi mwa barabara ili kuviruhusu vyombo vyenye kasi kupita.
  • Ukitaka kupita chombo kilichopo mbele yako tumia upande wa kushoto kukipita. Kua muangalifu na hakikisha chombo hicho hakijaonyesha ishara ya kukata kona kuingia upande wa kushoto.
  • Ukitaka kukata kona kuingia barabara ndogo au upande wakushoto mwa barabara, nyoosha mkono wako wakushoto kuelekeza upande huo ili kutoa ishara kwa aliekua nyuma yako.
  • Endesha kwa ustaarabu, na usitumie mwendo mkali utakaoweza kukupotezea udhibiti wa chombo chako.
  • Usipakie mzigo mzito na mkubwa utakaokuweka katika hatari uwapo barabarani.
  • Usipakie abiria zaidi ya mmoja kwenye baiskeli. Pia, usipakie abiria kwenye upande wa mbele wa kaiskeli.
  • Chukua tahadhari na kuwa makini wakati wote uwapo barabarani. Usiweke dhana kwamba watumiaji wengine wa barabara, hasa wale wenye vyombo va moto kua wanakuona.
PESACO TANZANIA