PESACO

PESACO ni shirika lisilo la kiserikali linalofanya shughuli zake Tanzania bara, likidhamiria kuhimiza jamii inayohiarika kufuata sheria bila shuruti. Dira yetu ni kufikia jamii salama inayohiarika kufuata sheria na kutoa ushirikiano kwa ajili ya usalama wake. Dhamira yetu ni kutoa elimu ya utekelezaji wa sheria, kukuza na kupanua uelewa wa jamii ili kupunguza na kuzuia uhalifu na matukio ya usalama barabarani.

Usalama Barabarani

Tunaelimisha jamii juu ya matumizi salama ya barabara ili kupunguza ajali na matukio ya usalama barabarani

Soma Zaidi
Matumizi Salama ya Mtandao

Tunaelimisha jamii kuhusu matumizi salama ya mtandao ili kuepuka uhalifu na matukio ya mtandaoni

Soma Zaidi
Jamilifu

Tunahimiza ushiriki wa jamii na juhudi za pamoja katika kuzuia uhalifu na kutambua viashiria hatarishi vya usalama

Soma Zaidi

Makala za Elimu

Elimika nasi

Mother, father with son and daughter in town.
Kumlinda Mtoto Dhidi ya Ajali Barabarani


Watoto wadogo huhitaji msaada kutoka kwa watu wakubwa pindi wakiwa kwenye mazingira ya barabara. Pia ni fursa kwao kujifunza kwa vitendo kuhusu mazingira na mienendo ya barabarani wakiwa na wakubwa wao, wazazi au walezi.Watoto wadogo hujifunza mienendo ya barabarani kwa kuangalia na kufanya au kuigiza kama watu wengine wafanyavyo. 

Soma Zaidi
IMG_0538
Mambo Yakuzingatia kwa Mtembea kwa Miguu Awapo Barabarani


Kila mtu ana upendeleo wake likija swala la usafiri, ila ukweli ni kwamba kila mmoja hutumia miguu kama usafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine, “every one is naturally a pedestrian”. Barabara sio kwa ajili ya magari na pikipiki pekee bali hata waenda  kwa miguu. Takwimu zinaonyesha kua waenda kwa miguu ni miongoni mwa wahanga wakubwa wa ajali za barabarani. 

Soma Zaidi
Screenshot_20211202-130704
Matumizi ya Taa za Barabarani


Taa za barabarani ni moja ya ishara za usalama barabarani na zipo kwa mujibu wa sheria ya usalama bararani sura ya 168 ya mwaka 2002. Taa za barabarani maranyingi hufungwa pembeni, au katikati ya barabara kwa lengo la kuongoza mserereko wa magari barabarani pamoja na kuweka uwiano sawa wa matumizi ya njia kwa makundi yote ya watumia barabara, kama wenye vyombo vya moto, waenda kwa miguu, waendesha baiskeli, wasukuma mikokoteni. 

Soma Zaidi