PROACTIVE LAW ENFORCEMENT FOR SAFE COMMUNITY Matumizi Salama Ya Mtandao
Matumizi Salama Ya Mtandao

Teknolojia ya habari na mawasiliano pamoja na matumizi ya mtandao kwa ujumla vimekua chachu ya maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa sio tu kwa Tanzania bali kwa dunia kiujumla. Mbali na umuhimu wa sekta hii katika maendeleo, matumizi mabaya ya teknolojia yamekua yakiathiri watu pamoja na vitu na kusababisha hasara kwa serikali na watu binafsi.

 

Idadi ya watu wanaotumia mtandao duniani imekua ikiongezeka siku hadi siku. Takwimu zinaonyesha hadi kufikia januari 2021 idadi ya watu wanaotumia mtandao ilifa bilioni 4.66 ambayo ni sawa na asilimia 59.5 ya watu wote duniani. Ongezeko hili la watumiaji wa mtandao, linaenda samabamba na ongezeko la uhalifu wakimtandao na madhara yatokanayo na matumizi mabaya ya mtandao. Tafiti zinaendelea kuonyesha kua kwa mwaka 2021 uhalifu wa kimtandao unaigharimu dunia dola zakimarekani trilioni 6, na huku ikizidi kukaridriwa kufikia dola trilioni 10.5 ifikapo mwaka 2025.

 

Kwa Tanzania, takwimu za TCRA zinaonyesha zaidi ya nusu ya watanzania wanatumia mtandao. Takwimu za taaisi ya taifa ya takwimu na jeshi la polisi zinaonyesha matukio ya uhalifu kwa njia ya mtandao yaliyo ripotiwa kwa mwaka 2020 ni 4,850 ikilinganishwa na matukio 3,514 yaliyoripotiwa kwa mwaka 2019. Likiwa ni ongezeko la matukio 1336. Uhalifu wa kimtandao husababisha hasara na madhara makubwa kwa watumiaji na serikali kwa ujumla.

 

Athari nyingi zitokanazo na matumizi ya mtandao husababishwa na mambo mawili. Moja ni uelewa mdogo kuhusu matumizi salama ya TEHAMA na mtandao kwa ujumla. Mbili ni kuzuka kwa mbinu mpya za uhalifu na wahalifu ambao wanatekeleza makosa kwa njia ya mtandao. Jeshi la polisi linaeleza “Kutokana na kukua kwa sayansi na teknolojia, wahalifu wamekuwa wakibuni mbinu mbalimbali za uhalifu na kusababisha kuibuka kwa aina mpya ya uhalifu kama makosa kwa njia ya mtandao…”

 

Sera ya taifa ya TEHAMA ya mwaka 2016 inatoa mwongozo juu ya matumizi na umuhimu wa teknolojia katika maendeleo, huku ikitambua athari za matumizi mabaya ya TEHAMA na kuhimiza utungwaji wa sheria na usimamizi thabiti utakao hakikisha uwepo wa usalama wa vitu na watu wanapotumia mtandao.

 

Ili kuilinda jamii na athari hasi zinazotokana na matumizi ya mtandao, juhudi za pamoja zimekua zikitumika hasa katika utoaji wa elimu juu ya matumizi salama ya mtandao. Serikali kupitia tasisi zake kama TCRA na Polisi, imekua ikifanya juhudi mbalimbali kama utungaji wa sheria, kanuni na sera mbalimbali zinazojikita katika kujinaisha matumizi mabaya ya mtandao, lakini pia kutoa elimu na kukuza uelewa juu ya usalama wa mtandao.

 

Mbali na juhudi za serikali, asasi za kiraia zina mchango mkubwa kuelimisha jamii na kukuza uelewa juu ya matumizi salama ya mtandao. Kwa kutambua hili, dhamira ya PESACO ni kuunga mkono jitihada za serikali na taasisi zake katika kuelimisha jamii juu ya matumizi salama ya mtandao.

 

  Njia Tunazozitumia Kutoa Elimu

  1. Kuita na kuandaa semina za elimu kwa makundi mbalimbali katika jamii, ikiwemo watoto na wazazi. Elimu hii inatolewa moja kwa moja kwa kufika maeneo husika;
  2. Kushirikiana na tasisi binafsi zikiwemo zile zinazolinda na kuhimiza maadili katika jamii, (mf. taaisi zakidini);
  3. Kushirikiana na serikali pamoja na taasisi zake (mf. TCRA na Polisi)
  4. Kufika kwenye shule za msingi na sekondari kwa lengo la kuwapa wanafunzi na walimu elimu, ujuzi na maarifa juu ya matumizi salama ya kompyuta;
  5. Kufika ofisi za serikari na binafsi kwa lengo la kutoa vitabu, vipeperushi na makala elimishi;
  6. Kuandaa vitabu, makala na vipeperushi elimishi
  7. Kutumi mitandao ya kijamii na vyombo vya habari
  8. Kuchapisha makala elimishi takitaka tovuti ya PESACO