UBAGUZI MTANDAONI NI KOSA KISHERIA
UBAGUZI MTANDAONI NI KOSA KISHERIA
Kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii hasa Facebook, Instagram na Twitter ni ukweli usiopingika kuwa huwa tunakutana na posti za kibaguzi. Mfano kuwatukana au kuwatania kabila fulani au dini fulani kwa utani mbaya au unaoudhi na kuumiza hisia za wahusika. Ubaguzi wa namna yeyote ile kwa kutumia simu au compyuta ni kosa kisheria chini ya sheria ya makosa ya kimtandao ya mwaka 2015. Sheria kupitia kifungu cha 17 inakataza mambo yafuatayo;
  1. Kuzalisha au kutengeneza maudhui au vitu vya kibaguzi kwa lengo la kuvisambaza mitandaoni au kwingineko
  2. Kutoa au kuwezesha upatikanaji wa maudhui ya kibaguzi
  3. Kurusha au kusambaza maudhui ya kibaguzi kupitia simu au kompyuta
Sheria imetoa adhabu kwa mtu yeyote atakaejihusisha na matendo hayo matatu au mojawapo ya hayo. Kama tulivyoona hapo juu hata kusambaza ujumbe au maudhui ya kibaguzi tayari nawe umefanya ubaguzi. Adhabu yake ni faini isiyopungua shilingi milioni tatu au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua mwaka moja au vyote kwa pamoja PESACO tunawasihi sana watanzania kujiepusha na matendo yeyote ya kibaguzi mtandaoni.

One thought on “UBAGUZI MTANDAONI NI KOSA KISHERIA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Shirika La Elimu ya Utekelezaji wa Sheria