Matumizi ya Mkanda wa Usalama na Mfuko wa Hewa (Seat belt & Air bag)
Matumizi ya Mkanda wa Usalama na Mfuko wa Hewa (Seat belt & Air bag)

Mkanda wa usalama na mfuko wa hewa ni vifaa vya kwanza kabisa vya kukuweka salama endapo ajali itatokea. Vifaa hivi vimewekwa kwa lengo kuu la kumzuia mhusika asiweze kujipigiza kwenye kioo cha mbele au asirushwe nje endapo ajali itatokea. Kwa mtu aliewahi kupata ajali, anaweza kukumbuka kwamba mwili wake ulivutwa kuelekea sehemu ya mgongano kati ya chombo chake na kingine. Katika mazingira haya ni mkanda wa usalama na mfuko wa hewa pekee vitakavyoweza kumsaidia kama alifunga mkanda. Mfuko wa hewa  unalinda kichwa, shingo, na kifua endapo ajali itatokea na gari likiwa kwenye mwendo kasi.   


  Faida za kufunga mkanda wa usalama na mfuko wa hewa

  1. Mkanda wa usalama huzuia mwili wako usirushwe nje ya gari
Watu wengi husema kuwa kama gari langu lina mfuko wa hewa sina sababu ya kufunga mkanda wa usalama, lakini kumbe wanasahau kuwa mfuko wa hewa hautakuwa na faida kwao endapo ajali itatokea. Kwahiyo faida ya kwanza ya mkanda wa usalama ni kumzuia dereva au mtu yeyote ndani ya gari asichomoke kwenye kiti chake na hatimaye kurushwa nje ya gari au kujipigiza kwenye vyuma au kitu kingine ndani ya gari. Mtu aliyefunga makanda wa usalama ana nafasi kubwa ya kutopata majeraha makubwa au kuumia sana kuliko yule amabaye hajafunga mkanda wa usalama endapo ajali itatokea.  

 
2. Mkanda wa usalama humzuia dereva kwenye kiti kwa namna ambayo mfuko wa hewa utamkinga na madhra makubwa endapo ajali itatokea 

 Mkanda wa usalama utamzuia dereva au abiria asichomoke kwenye kiti endapo ajali itataokea. Kwa upande mwingine mfuko wa hewa ambao upo kwenye usukani kwa ajili ya dereva na  kwenye dashibodi kwa ajili ya abiria utafanya kazi ya kupunguza athari na  kumkinga dereva/abiria na kitu chochote amabacho kingerushwa kwa uelekeo wake au dereva/abiria mwenyewe kurushwa kuelekea kitu chochote ambacho kwa namna moja ama nyingine kingemdhuru. Mfuko wa hewa utafanya kazi yake vizuri kama dereva au abairia amefunga makanda.       


3. Hupunguza hatari ya kupata majeraha makubwa zaidi au kifo 

 Wapo watu wengi walionusurika kufa au kuumia vibaya kwakua walikuwa wamefunga mkanda wa usalama mbali na kuwa walipata ajali kubwa. Endapo mtu atapata ajali kubwa au ndogo nafasi ya kutokuumia vibaya inaongezeka kama mtu huyo atakua amefunga mkanda wa usalama kuliko yule ambaye hajafunga mkanda huo.       


4. Inapunguza usumbufu wa kusimamishwa na askari wa usalama barabrani na adhabu zinazokwepeka kirahisi 

 Tufahamu kwamba kanuni na sheria za usalama barabarani zinamtaka dereva na abiria kufunga mkanda wa usalama, kama mtu hujafunga mkanda huo atakuwa umevunja sheria na atakuwa umeingia kwenye ugomvi na watu wa mamlaka za usimamizi wa sheria. Hivyo ili kujiepusha na adhabu au usumbufu usiokuwa wa lazima ni vyema kufunga mkanda wa usalama kwenye gari       


5. Mfuko wa hewa unakinga kifua,shingo na kichwa dhidi ya majeraha makubwa ajali inapotokea

 Mfuko wa hewa hujaa hewa mara pale tu ajali inaopotokea na kusaidia kifua chako, shingo na kichwa kutokupata madhara makubwa. Mfuko wa hewa unakuwa kama godoro kukinga kichwa, shingo au kifua kisiumie. Lakini pia mfuko wa hewa humzuia dereva au abiria asirushwe nje ya gari au kichwa chake kisipigize na kitu kingine ndani ya gari.

Shirika La Elimu ya Utekelezaji wa Sheria