kampeni hii inalenga kuhakikiasha wanafunzi hasa wa shule za msingi na sekondari wanapata elimu stahiki ya usalama barabarani. Malengo hasa ya PESACO kuanzisha kampeni hii ni;
- Kuwajengea wanafunzi tabia na desturi za kuzifahamu, kuziishi na kuzitekeleza sheria, taratibu na kanuni za usalama barabarani tangu wakiwa wadogo
- Kuzifahamu na kuzitumia ipasavyo alama na michoro ya barabarani
- Kuimarisha na kusissitiza mitazamo chanya wakati wa kutafsiri mazingira hatarishi barabarani,
- Kuwajengea wanafunzi uwezo wa kujilinda binafsi na kuwalinada watumiaji wengine wa barabara pindi wawapo barabarani.