FAHAMU VYANZO VYA AJALI BARABARANI
FAHAMU VYANZO VYA AJALI BARABARANI
Ajali barabarani ni jambo ambalo hua ni tishio kwa watumiaji wote wa barabara japokuwa hutokea na kujirudia mara kwa mara. Kwa bahati mbaya zaidi hatujifunzi kutokana na makosa yetu tunayofanya kilasiku tunapotumia barabara. Uhaba wa uelewa wa kutosha juu ya elimu ya usalama barabarani pamoja na mapuuza ya watumiaji wa barabara ni sababu kuu inayosababisha ajali nyingi kutokea. Kuna vyanzo vikuu vitatu vya ajali;
  1. Makosa ya kibinadamu
  2. Miundombinu ya barabara
  3. Hali ya hewa na chombo chenyewe
 
  1. MAKOSA YA KIBINADAMU
Yapo makosa mbalimbali yanayofanywa na binadamu au watumia barabara ambayo hupelekea ajali kutokea. Makosa haya hufanywa na makundi kama madereva, watembea kwa miguu, waendesha baiskeli na maguta kwa uchache. Hata hivyo madereva wa vyombo vya moto hua ndio chanzo kikubwa cha ajali. Yafuatayo  ni baadhi ya matendo yanayopelekea kutokea kwa ajali. Mwendo mkubwa Ajali nyingi na mbaya maranyingi hutokea kutokana na mwendo kasi wa dereva. Madereva wengi wakiwa barabarani huendesha kwa mwendo mkubwa sana na wengine huendesha kwa ashiki na mihemko ambayo madhara yake ni ajali. Vikundi vyote vya watumia barabara hutumia barabara kwa wakati mmoja hivyo ni lazima wakati mwingine kutumia barabara kwa zamu na kutoa nafasi au kuwa na subira pale mtu mwingine anapotumia barabara. Kuendesha kwa mwendo mkubwa barabarani huzidisha nafasi ya kupata ajari mara mbili ya yule anaeendesha kwa mwendo wa kawaida na pia kupelekea madhara kuwa makubwa zaidi pale ajali inapotokea. Magari ya mwendo mkubwa maranyingi ndiyo amabyo hupata ajali na madhara yanayotokea huwa makubwa zidi kuliko ile amabayo ingewapata wale wanaoendesha kwa mwendo mdogo. Kadri mwendo wa gari unavyokuwa mkubwa vivyo hivyo hatari pia huwa kubwa. Gari linaloendeshwa kwa mwendo mkubwa huhitaji umbali mrefu ili liweze kusimama yaani umbali wa kushika breki. Gari linaloendeshwa kwa mwendo mdogo husimama haraka na kwa umbali mfupi wa breki na mserereko wake nimfupi kuliko linaloendeshwa kwa mwendo mkubwa. Kwa gari linaloendeshwa kwa mwendo mkubwa uwezo wa kufanya maamuzi kwa haraka unapungua kwa dereva na pia uelewa na kutafsiri mazingira hatarishi pia hupungua. Hivyo madereva wote wawapo barabarani wanapaswa kuendesha vyombo vyao kwa kuzingatia vizibiti mwendo na alama zote zilizopo bararabarani.   Matumizi ya vilevi Kunywa pombe na kufurahia maisha ni jambo la kawaida na wala si kosa. Lakini unapolewa na kuendesha chombo cha moto hapo kitendo hicho hubadilika nakuwa kosa, na zaidi ya kuwa kosa linaweza kugharimu maisha yako kama dereva au maisha ya watu wengine. Pombe hupunguza umakini wa dereva barabarani. Huchelewesha mtiririko wa taaarifa katika mwili wa mtu. Miguu huchelewa kutekeleza taarifa kutoka kwenye ubongo. Dereva hupata uono hafifu kutokana na kizunguzungu kinachotokana na pombe. Pombe huondoa hofu na kupelekea mtu kufanya jambo hatarishi. Haya yote hupelekea ajali kipindi unaendesha ukiwa umelewa na maranyingi ajali huwa kubwa na mbaya zaidi. Mbali na ulevi wa pombe zipo dawa mbalimbali zinazopunguza ujuzi na umakini wakati wa kuendesha. Madereva hushauriwa kutokunywa pombe na kuendesha. Pia ukitumia dawa inayokupelekea uchovu wa mwili na viungo basi usiendeshe chombo cha moto. Vizuizi kwa dereva Vizuizi kwa dereva huchangia ajali kwa kiasi kidogo lakini inaweza kusababisha ajali kubwa. Vizuizi vinaweza kutoka nje au ndani ya chombo husika. Kizuizi kikubwa sana ni kutumia simu wakati wa kuendesha. Sehemu kubwa ya fikra na umakini huhamia kwenya mazungumzo ya simu na sehemu ndogo iliyobakia hutumika kuendesha chombo. Mgawanyiko huu wa akili na umakini hupelekea kuchelewa kufanya maamuzi kwa haraka na hatimaye ajali kutokea. Madereva hushauriwa kuweka mbali simu zao wakati wa kuendesha na kutozungumza na simu au kutumiana jumbe wakati wa kuendesha. Endapo simu hiyo itakuwa ya lazima kupokea basi toka pepembeni ya barabara upaki na uzungumze. Madereva wanashauriwa kutojihusisha na chochote nje na lengo la kuwa bararabarani na kuendesha kwa mwendo salama ili kuwa salama barabarani na kutoruhusu umakini wao na akili zikachukuliwa na vitu vingine.   Kupuuza taa, alama na michoro ya barabarani Imekuwa ni mazoea siku hizi madereva kupuuza taa za barabarani na kukatiza bila kuzitilia maanani. Lengo la taa za barabarani ni kuongoza magari kusimama na kutoa nafasi ya mapokezano ya kutumia barabara kwa zamu na lengo kuu ni kuokoa muda barabarani. Tafiti nyingi huonesha kuwa uendeshaji unaofuata mwongozo wa taa za barabarani husaidai sana kuokoa mda barabarani na watumia barabara hufika mwisho wa safari salama na kwa wakati. Anaepuuza taa za barabarani siyo tu kuhatarisha maisha yake bali pia anahatarisha usalama wa watumiaji wengine wa barabaraba. Kupuuza huko kwa dereva mmoja hupelekea madereva wengine kuiga mfano huo mbaya na mwishowe kupelekea kero na usumbufu bararani. Kwamfano kwenye makutano ya barabara upuuzaji wa taa za barabarani husababisha msongamano wa magari na foleni isiyoyalazima. Kutofunga mkanada wa usalama na kutokuvaa kofia ngumu Ni kwa matakwa ya sheria kuwa ni sharti kufunga mkanda wa usalama (seat belt) kwa magari, na kuvaa kofia ngumu kwa waendesha pikipiki. Mkanda wa usalama na kofia ngumu husaidia kupunguza majeruhi na maafa makubwa endapo ajali itatokea. Mtu aliefunga mkanda wa usalama na alie vaa kofia ngumu ananafasi ya kunusurika na maumivu na maafa mara mbili zaidi ya yule ambae hajafunga mkanda au ambae hawajavaa kofia ngumu. Vifo vingi vinavyotokana na ajali za pikipiki vimepungua tangu matumizi ya kofia ngumu yalipowekwa kama takwa la sheria. Watu wote wanashauriwa kutumia mkanda wa usalama pamoja na kofia ngumu ipasavyo ili uweze kunusurika endapo ajali itatokea.   Kubeba mzigo unayozidi uwezo wa chombo Hiki ni kitendo cha chombo cha moto kubeba mzigo mkubwa unaozidi uwezo stahiki wa chombo hicho. Inafahamika kuwa kila chombo kinakuwa na kiasi maalum cha uwezo wake wa kubeba mzigo. Kwa mfano mabasi au magri binafsi yanakuwa na kiwango maalum cha idadi ya abiria au watu wa kubeba. Lakini madereva wengi hasa wa bajaji, bodaboda na daladala za vijijini hubeba abiria wengi zaidi ya uwezo wa chombo na hali hii hupelekea ajali kutokea kiurahisi. Kwa mfano kitendo cha bodaboda kubeba mishikaki ni hatarishi sana na kinapaswa kupingwa na kilamtu. Kubeba mzigo mkubwa kuliko uwezo wa gari hupelekea ajali kwasababu wakati mwingine dereva hushindwa kutawala chombo wakati wa hali ya dharuara hayo yote huongeza nafasi ya ajali kutokea.    
  1. MIUNDOMBINU YA BARABARA
Barabara pia huwa ni chanzo kimojawapo cha ajali. Kwa hapa dereva huumia bilakuwa na hatia yeyote upande wake. Barabara nyingi za vumbi huharibika kipindi cha mvua. Hali hii hupelekea magari kuteleza na kuharibika barabarani na hatimaye kusababisha ajali. Mazingira mengine ya barabara kuwa chanzo cha ajali ni pale  barabara kuwa nyembamba sana ajali inaweza kutokea endapo magari yatakutana yakiwa yapo kwenye mwendo mkubwa wakati wa kupishana ajali inaweza kutokea. Mashimo na bamsi nyingi bararabani yanaweza kuwa chanzo cha ajali. Mazingira yote magumu ya barabara husababisha dereva kushindwa kutawala chombo chake na kupelekea ajali.  
  1. HALI YA HEWA NA CHOMBO CHENYEWE
Hali ya mazingira inaweza kuwa chanzo cha ajali. Mfano uwepo wa ukungu, theluji, mvua kubwa, kimbunga au upepo mkali. Wakati mwingine chombo chenyewe kinaweza kuwa sababu ya ajali. Mfano  breki kufeli, steling kung’ooka, gurudumu kubasti, n.k

One thought on “FAHAMU VYANZO VYA AJALI BARABARANI

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

PESACO TANZANIA